Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu kuijadili Syria

Baraza la haki za binadamu kuijadili Syria

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuandaa mjadala wa dharura kuhusu mzozo wa kisiasa unaondelea nchini Syria juma lijalo. Ombi la kutaka kuandaliwa kwa mjadala huo lilitolewa na taifa la Qatar na kuungwa mkono na wanchama kadhaa wa baraza hilo wakiwemo Marekani, Jumuiya ya Ulaya na mataifa kadhaa ya kiarabu.

Hiyo jana tume ya uchunguzi iliyoteuliwa na baraza hilo kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Syria ilitoa ripoti yake ambapo inaishutumu serikali ya Syria kwa kukiuka haki za binadamu hadi kufikia kiwango cha kutajwa kuwa uhalifu dhidi ya ubidamu. Ripoti hiyo inasema kuwa dhuluma ziliendeshwa huku serikali ikielewa wazi. Rais wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Laura Dupuy Lassere anasema kuwa ana matumaini kuwa mkutano huo utajadili hali inayoendelea kuzorota nchini Syria na kutaka kukomeshwa kwa ghasia.