Kuuimarisha utawala wa sheria ni muhimu sana:Migiro
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa kujihusisha katika kuimarisha utawala wa sheria, jambo ambalo limeleta matunda yaliyoshuhudiwa katika nchi mbalimbali hasa kuchagiza uwajibikaji na uwazi.
Akizungumza kwenye kamati ya Baraza Kuu inayoshughulika na masuala ya sheria ambayo pia hujulikana kama Sixth Committee au kamati ya sita, Asha-Rose Migiro amegusia hamu ya watu kote duniani ya kutaka kuwa na serikali zinazozingatia utawala wa sheria.
Amesema matukio yaliyojitokeza Afrika ya Kaskazini na Maashariki ya Kati mwaka huu yanakumbusha nia ya kimataifa ya watu kutaka kuwa na utawala wa sheria na sio wa watu.
Bi Migiro amesema jukumu la muda mrefu la kamati ya sita limekuwa muhimu sana katika kuhakikisha utawala wa sheria unaadimishwa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.