Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda 2030 ni lazima itambue mchango wa wanawake- Mkuu wa UN Women

Ajenda 2030 ni lazima itambue mchango wa wanawake- Mkuu wa UN Women

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, Phumzile Mlambo-Ngcuka, ametoa wito kwa kila mmoja ashiriki katika kampeni ya kuwawezesha wanawake na kufikia usawa wa jinsia, ili kutimiza  ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu. Taarifa kamili na Flora Nducha

Taarifa ya Flora

Sauti

Ndivyo hali ilivyokuwa katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu huyo wa UN Women amesema ajenda 2030 ina dhamira ya kutomwacha mtu yeyote nyuma, na kwamba wanawake na wasichana wanaweza, na ni lazima wawe na mchango muhimu katika kutimiza malengo ya ajenda hiyo.

“Tunatoa wito kwetu sote tujiunge kwa pamoja katika kampeni ya #StepItUp na kuhakikisha kuwa tunachukuwa jukumu la kufikia usawa wa jinsia ifikapo mwaka 2030, na mabadiliko makubwa na ya kudumu, ifikapo mwaka 2030”

Bi Mlambo Ngcuka amesema ajenda ya maendeleo endelevu inahusu nguvu ya ajenda jumuishi, inayomhusu kila mtu.

Ameongeza kuwa siku hii ni wakati wa kuadhimisha hatua zilizopigwa katika kuwawezesha wanawake, na kufanya mabadiliko katika jinsi tunavyoishi na kufanya maendeleo