Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wana wajibu mkubwa wa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake: Ban

Polisi wana wajibu mkubwa wa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake: Ban

Akwia ziarani  nchini Algeria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefungua mkutano kuhusu ukomeshwaji wa ukatili dhidi ya wanawake uliopewa jina Kigali, akipigia chepuo haki za wanawake hususani barani humo. Priscilla Lecomte na taarifa kamili.

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Katika hotuba yake Ban amesema harakati za ukombozi wa wanawake zinachagizwa na makataba wa Afrika kuhusu haki za binadamu ambao unapiga marufuku unayanyasaji, ukatili, udhalilishaji na adhabu.

Katibu Mkuu amesema mkataba wa kuondoa aina zote za ubauzi dhidi ya wanawake ambao umesainiwa na nchi nyingi baraniAfrika pia huwekea  msisitizo zaidi juu ya haki za wanawake katika kuishi maisha ya uhuru dhidi ya ubaguzi na ukatili na akazungumzia umuhimu wa polisi katika utekelezaji wa hili akisema.

(SAUTI BAN)

‘Polisi wanaweza kusaidia kupinga ukatili na ukwepaji sheria . Wanafanya kazi na wadau wa mahakama, kuchunguza tuhuma, kudhihirisha watuhumiwa, kukuza uwajibikaji na kuhakikisha wahanga wanapata matibabu.’’