Waganga wa kienyeji Kenya kuwajibika kisheria kwa tiba zao- Ripoti

25 Februari 2016

Kikao cha 57 cha makubaliano ya kimataifa ya haki za uchumi, kijamii na utamaduni kinaendelea mjini Geneva Uswisi na leo Alhamisi miongoni mwa nchi zilizowasilisha ripoti yake ni Kenya. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA )

Ikiwasilisha ripoti  yake kwenye kikao hicho Kenya imesema upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo maji safi,  elimu na afya unakabiliwa na changamoto licha ya hatua muhimu zilizopigwa.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa hii, mwakilishi wa ujumbe wa Kenya  kwenye mkutano huo Dr. Pasifica Onyancha kutoka wizara ya afya, amesema kwamba kwa sasa huduma za afya zinapatikana katika kilometa tano kwa kila mwananchi katika pembe zote za nchi lakini….

(Suati ya Dr.Onyancha)

Kwa mantiki hiyo serikali imechukua hatua kupitia sheria ya afya mpya ili kuhakikisha kwamba waganga wa kienyeji wanawajibika kisheria.

(Sauti ya Dr. Onyancha)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter