Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 22,000 wapata vitambulisho Afrika Magharibi

Zaidi ya watu 22,000 wapata vitambulisho Afrika Magharibi

Leo ikiwa ni mwaka mmoja tangu kupitishwa kwa azimio la Abijan kuhusu kutokomeza ukosefu wa kutokuwa na utaifa, tayari zaidi ya watu 22,000 wamepewa vitambulisho vya uraia kwenye ukanda wa Afrika Magharibi. John Kibego na taarifa kamili.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR likikaribisha mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka huu mmoja,huku baadhi ya serikali za ukanda huo zikiwa zimechukua hatua za kisheria kupambana na tatizo hilo.

UNHCR imeeleza kwamba bado watu wapatao milioni moja hawana utaifa au wako hatarini kukosa utaifa Afrika Magharibi, hali hii ikiweza kuathiri uwezo wao wa kupata huduma za elimu, afya, ajira na ardhi.

Watoto wanaoishi barabarani hawasajiliwa wakati wa kuzaliwa na hivyo wako hatarini zaidi kuteseka na kutumikishwa na wahalifu, limeongeza shirika hilo.