Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM imebaini, ukiukaji, unyanyasaji na kuongezeka kwa machafuko Libya:

Ripoti ya UM imebaini, ukiukaji, unyanyasaji na kuongezeka kwa machafuko Libya:

Libya ipo katika mtego wa kutumbukia kwenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao unaweza kuwa uhalifu wa kivita huku hali mbaya ikiongezeka kwa kasi miongoni mwa watu Umoja wa Mataifa umesema Alhamisi.

Ikitangaza matokeo ya ripoti mpya kuhusu ukiukwaji wa haki kwenye nchi hiyo iliyoathirika na vita , ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetanabaisha kwamba pande zote kinzani nchini humo zinawajibika.

Miongoni mwa mapendekezo, ripoti inatoa wito kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kupewa uwezo wa kuchunguza na kuwafungulia mashitaka wale wote waliohusika kwa mauaji katika taifa hilo la Afrika ya Kaskazini.