Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya Sudan Kusini yawatawanya 26,000 Malakal:UNHCR

Mapigano mapya Sudan Kusini yawatawanya 26,000 Malakal:UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linahofia kwamba watu takribani 26,000 wametawanywa na mapigano mapya yaliyozuka Jumatano jioni wiki hii kati ya kabila la Dinka na Shilluk kwenye kituo cha wakimbizi wa ndani mjini Malakal Sudan Kusini.  Grace Kaneiya na taarifa Zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Shirika hilo limesema Alhamisi wanajeshi wa Sudan’s People Liberation Army (SPLA) wamearifiwa kuingia katika eneo la ulinzi wa raia linalohifadhi wakimbizi wa ndani 48,000, huku washirika wa utoaji wa misaada ya kibinadamu katika enero hilo wakitoa taarifa za milio ya risasi, uporaji na kuchomwa kwa nyumba.

Nao wafanyakazi wa UNHCR wanasema raia wanakimbia wakibebaba chochote wawezacho na wale wasiojiweza wakiachwa nyuma, huku watoto wakipotezana na familia zao. Andreas Needham, ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ANDREAS NEEDHAM)

"Wahudumu wa kibindamu wameripoti ufyatuliwaji risasi, uporaji na kuteketezwa kwa nyumba. Tunashirikiana na waliokimbia makwao kugawa misaada. Majadiliano yanaendelea na hali inabadilika kila uchao. Tunamatumaini kwamba kutakuwa na matokeo mazuri na yenye amani kwa ajili ya watu wengi waliofurushwa makwao na kukimbilia ndani na nje mwa nchi."