Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati kura zikihesabiwa Uganda, kiongozi wa upinzani atiwa ndani:

Wakati kura zikihesabiwa Uganda, kiongozi wa upinzani atiwa ndani:

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa nchini Uganda imethibitisha kuwa, wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea nchini Uganda kufuatia uchaguzi mkuu wa Alhamisi wiki hii, kiongozi wa upinzani nchini humo Dr Kiiza Besigye amekamatwa na wafuasi wake kutawanywa kwa mabomu ya kutoa machozi. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa mwakilishi wa ofisi ya haki za binadamu nchini humo. Bwana Uchenna Emelonye kiongozi huyo wa upinzani alikuwa kwenye ofisi za chama chake polisi walipovamia na kumtia nguvuni. Ameongeza kwamba…

(SAUTI YA UCHENNA)

“Hali ya leo inayotia wasiwasi ni kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Dr Besigye kwenye ofisi yake walikuwa wamekusanyika kuhesabu kura na labda polisi walidhani wamekutana kutangaza matokeo tofauti na yale ynayotolewa na tume ya uchaguzi waka mkamata na kutawanya wafusi wake.”

Ameongeza pia polisi walituimia risasi kuwatawanyavijana mjini kampala ambapo kuna taarifa za majeruhi na vifo lakini hawezi kuthibitisha ni watu wangapi walioathirika na tukio hilo. Kwa upande mwingine amesema tume ya uchaguzi inaendelea kuhesabu kura na matokeo ya awali yanashiria Rais aliyeko madarakani Yopweri Kaguta Museveni anaelekea kushinda.