Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Theluthi ya Wairaq wanahitaji msaada: UNAMI

Theluthi ya Wairaq wanahitaji msaada: UNAMI

Takribani theluthi moja ya Wairaq wote wanahitaji hara msaada wa kibinadamu kwa mujibu wa mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNAMI. Bwana Ján Kubiš ameyasema hayo Jumanne alipotoa taarifa kwenye baraza la usalama akiongeza kuwa majeshi ya Iraq yamekuwa shujaa kwa kuweza kulishinda nguvu kundi la ISIL katika baadhi ya maeneo, lakini ukosefu wa muafaka wa kisiasa umekuwa kikwazo kwa juhudi za kitaifa. Ameongeza kuwa wanaoteseka zaidi ni mamilioni ya wakimbizi wa ndani

(SAUTI YA KUBIS)

"Leo hii sio tuu wakimbizi wa ndani milioni 3.3 , lakini kwa pamoja Wairaq milioni 10 karibu theluthi ya watu wote wanahitahi msaada wa haraka wa aina Fulani. Bila msaada wa lazima wakimbizi wa ndani wa leo watakuwa wakimbizi wa kesho. Mahitaji ya kibinadamu ni makubwa mno yashinda uwezo wa kitaifa kuyakabili.”

Bwana Kubiš pia ametumia wakati huo kulaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa UNAMI yaliyothibitishwa Jumanne. Amer a-Kaissy alikuwa afisa ushirikiano wa UNAMI kwenye jimbo la Diyala. Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa akizungumzia kifo chake amesema kikimekuwa cha kustusha sana na ametoa wito wa uongozi wa Iraq kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wahusika.