Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza tena kuwakwamua wahamiaji wa Kiethiopia kutoka Yemen

IOM yaanza tena kuwakwamua wahamiaji wa Kiethiopia kutoka Yemen

Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanzisha upya operesheni zake za ukozi kwa wahamiaji wa Ethiopia walikwama huko Yemen.

Zoezi hilo ambalo linafadhiliwa na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha kukabili majanga ya dharura, linatazamia kuwafaidia watu 2,400 ambao katika kipindi cha wiki kadhaa watakuwa wamerejea makwao.

 

Kundi la kwanza la watu 120 ikiwemo watoto na wazee linatazamiwa kuwasili mjini Addis Ababa kesho jumamosi ambapo baada ya hapo watatawanywa kwenye maeneo yao ya asili.

 

Hapo mwanzo IOM ilifanikiwa kuwakwamua wahamiaji wengine 2,770 waliokwama katika eneo la Kaskazini mwa Yemen katika kipindi cha mwenzi Novemba hadi February mwaka huu. Operesheni hiyo ilisimama kutokana kukosekana kwa fedha.