Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Soko la madini ya chuma ghafi lilishuka katika mwaka 2015

Soko la madini ya chuma ghafi lilishuka katika mwaka 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo, UNCTAD, limesema leo kuwa mwaka 2015 ulikuwa mgumu kwa soko la madini ya chuma ghafi, kutokana na kuendelea kwa ongezeko la uzalishaji,  pamoja na mahitaji madogo ya madini hayo.

Ripoti ya UNCTAD kuhusu chuma ghafi ya mwaka 2015, inamulika soko la chuma ghafi kutoka mwaka 2014 na mwelekeo katika miaka ya 2015-2016, ikionyesha kuwa uzalishaji mdogo wa chuma kote duniani uliathiri soko la chuma ghafi, kwani bei yake ilishuka mno na hivyo kushusha faida za kampuni za kuchimba migodi.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa uzalishaji wa chuma duniani ulikuwa tani milioni 1,763 mwaka 2015, ukiwa umeshuka kwa asilimia 2.9, huku uzalishaji wa chuma ghafi ukiwa tani 1,948, ukipungua kwa asilimia 6 kutoka mwaka 2014.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNCTAD, bei ya chuma ghafi imeshuka sana na kufikia kiwango ambacho hakijaonekana tangu mwaka 2002, ambapo kulikuwa na ukuaji wa kasi wa soko la chuma ghafi.