Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi ya makombora Syria yanaweka wingu – Ban

Mashambulizi ya makombora Syria yanaweka wingu – Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia mashambulizi ya makombora kutoka angani dhidi ya shule na hospitali za watoto huko Syria na kusema kuwa tukio hilo linatia wasiwasi mkubwa.

Kupitia naibu msemaji wake, Farhan Haq, Ban amesema makombora hayo yaliyoripotiwa kutua kwenye vituo angalau vitano vya afya na shule mbili huko nchini Syria mjini Allepo yamesababisha vifo vya raia 50 wakiwemo watoto huku wengine wakiachwa na majeraha.

Amesema kitendo hicho ni kinazidi kusambaratisha huduma za afya ambazo tayari ziko kwenye hali mbaya, hali kadhalika zinakwamisha huduma ya elimu bila kusaha kuwa ni kinyume na sheria za kimataifa, lakini zaidi ya yote..

(Sauti ya Farhan)

“Matukio haya yanaweka wingu dhidi ya ahadi zilizotolewa na kikundi cha kimataifa cha usaidizi kwa Syria, ISSG wakati wa mkutano wao huko Munich Ujerumani tarehe 11 mwezi Februari.Lazima tutumie fursa hii ya makubaliano na kubadilisha kutoka kwenye kauli kuwa vitendo iwapo tunataka kujenga imani kwa kikundi hicho na kwa jamii ya kimataifa.”