Radio ya Umoja wa Mataifa ilitupatia sura mbadala ya harakati za ukombozi- Edda Sanga

13 Februari 2016

Miaka 70 ya Radio ya Umoja wa Mataifa inaadhimishwa leo wakati ambapo matangazo ya chombo hicho yamekuwa yakijikitaka katika kueneza majukumu ya msingi wa Umoja huo ikiwemo kuendeleza amani. Mathalani harakati za ukombozi barani Afrika hususan nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara zilikuwa sehemu ya matangazo ya Umoja huo kupitia idhaa zake ikiwemo ile ya Kiswahili. Matangazo hayo yalirushwa kupitia radio washirika ikiwemo Radio Tanzania Dar es salaam, sasa ikijulikana kama Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC. Edda Sanga mmoja wa watangazaji wakongwe nchini Tanzania na aliwahi kuwa mkuu wa mipango katika chombo hicho amweleza Assumpta Massoi wa Idhaa hii vile ambavyo matangazo hayo yalisaidia kuleta ukombozi.