Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Redio ya Umoja wa Mataifa imechangia kukuza Kiswahili- Abdillahi Zuberi

Redio ya Umoja wa Mataifa imechangia kukuza Kiswahili- Abdillahi Zuberi

Leo tarehe 13 Februari ni Siku ya Kimataifa ya Redio Duniani. Leo ni siku maalum pia, kwani Redio ya Umoja wa Mataifa inaadhimisha miaka 70 tangu azimio lililokianzisha chombo hicho adhimu cha kupasha habari na kubadilishana mawazo.

Redio ya Umoja wa Mataifa inatangaza kwa lugha nane, zikiwemo Kiswahili, Kireno na lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kirusi, Kichina na Kihispania.

Abdillahi Zuberi Rijal, mfanyakazi mstaafu wa Umoja wa Mataifa, ambaye zamani alikuwa mtangazaji na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa, alijiunga na idhaa hii mwaka wa 1978, akiwa bado mwanafunzi, akisomea shahada yake ya pili. Alipojiunga na Redio ya Umoja wa Mataifa, alianza kwa kufanya kazi na vitengo vya kupigania uhuru wa Namibia na kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Katika mahojiano na Joshua Mmali, anaanza kwa kuzungumzia vipindi walivyoandaa enzi zile