Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziarani Mali, Helen Clark aunga mkono juhudi za serikali

Ziarani Mali, Helen Clark aunga mkono juhudi za serikali

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, Helen Clark, yuko ziarani Mali hadi tarehe 9 Februari, ili kukariri msimamo wa UNDP wa kusaidia serikali ya Mali katika jitihada zake za kutimiza malengo ya maendeleo.

Katika ziara hii, Bi Clark anatarajiwa kukutana na rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, viongozi wa serikali, na wawakilishi wa mashirika ya kibinadamu.

Aidha atakuwa na mikutano na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa jamii.

UNDP inategemea kuongeza msaada wake kwa serikali ya Mali ili kuisaidia kutekeleza makubaliano ya amani na maridhiano nchini Mali yaliyosainiwa mwaka uliopita