Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya vikundi vya misimamo mikali ni lazima vianzie mashinani:Dkt. Ali

Vita dhidi ya vikundi vya misimamo mikali ni lazima vianzie mashinani:Dkt. Ali

Februari mosi hadi saba ni wiki ya kuadhimisha  uwiano baina ya imani mbalimbali za kidini ulimwenguni. Wiki hii ilitengwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kupitia azimio la tarehe 20 Oktoba mwaka 2010. Azimio hilo pamoja na mambo mengine linataja uelewa na mazungumzo baina ya dini mbalimbali kama kiungo muhimu katika kuimarisha maelewano miongoni mwa watu wengi licha ya Imani zao.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Dkt. Mustapha Ali ambaye ni Katibu Mkuu wa mtandao wa kimataifa wa dini kwa watoto, GNRC  ambapo katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumzia udhibiti wa misimamo mikali hususan miongoni mwa vijana. Hapa anaanza kwa kuelezea lengo kuu la mkutano.