Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Kenya ataka miradi pamoja na vijana si miradi kwa vijana - #Youth2030

Mwakilishi wa Kenya ataka miradi pamoja na vijana si miradi kwa vijana - #Youth2030

Mjini New York, Marekani, wawakilishi wa vijana kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekusanyika kushiriki kongamano la siku mbili la vijana lililoandaliwa na Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, ili kujadili namna ya vijana kujumuika kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Lengo la mkutano pia lilikuwa ni kuwapatia vijana jukwaa la kuzungumza na viongozi wa nchi zao kuhusu sera zinazolenga vijana na ajenda ya maendeleo, huku mwakilishi wa vijana akitakiwa kuwasilisha mapendekezo yao kwa Kamisheni ya Maendeleo ya Jamii inayoanza mkutano wake wa mwaka wiki hii. Miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo Lawrence Muli, raia wa Kenya, mfanyakazi wa Jumuiya ya Commonwealth na mtalaam wa maswala ya kisiasa.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte anaanza kumwelezea matarajio yake katika mkutano huo.