Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati kwingineko duniani wanawake wamepiga hatua kujikomboa Congo DRC bado inasuasua

Wakati kwingineko duniani wanawake wamepiga hatua kujikomboa Congo DRC bado inasuasua

Wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani tangu tarehe mosi March wanakutana hapa New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika Kikao cha 54 cha kimataifa cha wanawake kinachojadili hali ya wanawake duniani baada ya mkutano wa Beijing .Congo DRC bado inajikongoja.

Kikao hicho kutokana na maelezo ya wawakilishi mbalimbali kinasema hatua zimepigwa katika kumkomboa mwanamke japokuwa sio kwa asilimia mia moja Hata hivyo sio kila nchi duniani ambaye imetekeleza maazimio ya Beijing miaka 15 baada ya mkutano huo wa wanawake wa kimataifa uliofanyika mwaka 1995.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni miongoni mwa nchi ambazo maazio mio mengi ya Beijing yamewapita ubavu. Wanawake wengi bado hawana fursa sawa na wanaume katika ngazi za uongozi, masuala ya mirathi na hata umilikaji ardhi, japo wamejikongoja saana katika upande wa kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto wa kike.

Kuitathmini hali hiyo ya Congo miaka 15 baada ya mkutano wa Beijing nimezungumza na Mwalimu Dina Masika Yalala, ambaye pia ni mwanaharakati wa kupigania haki za wanawake na aliwahi kuwa naiabu waziri wa elimu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Anaoje maendeleo ya mwanamke nchini humo miaka 15 baada ya Beijing? Sikiliza mahojiano kamili kwenye tovuti hii.