Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwelekeo wa uwekezaji wa kigeni Afrika watia shaka 2016- UNCTAD

Mwelekeo wa uwekezaji wa kigeni Afrika watia shaka 2016- UNCTAD

Ripoti mpya ya kamati ya maendeleo ya biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kuhusu mwelekeo wa uwekezaji wa vitegauchumi wa kigeni duniani imeonyesha bayana kuzidi kudidimia kwa uwekezaji huo katika nchi za Afrika hususan zile zinazoendelea. Hata hivyo mataifa mengine yamenufaika kwa kupata uwekezaji mkubwa ambapo kwa ujumla yaelezwa kuwa uwekezaji huo duniani umeongezeka kwa asilimia 36 mwaka 2015. Je kwa ni nchi zipi zimenufaika zaidi? Sababu ni nini? Na mwelekeo ni upi unatarajiwa? Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi ambaye katika kufafanua kwa undani ripoti hiyo anaanza kwa muhtasari kile kilichobainika.