Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Somalia na Ethiopia watumikishwa Yemen

Wahamiaji wa Somalia na Ethiopia watumikishwa Yemen

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Yemen, Johannes van der Klaauw, ameeleza kwamba baadhi ya watu waliokimbilia Yemen kutoka Somalia na Ethiopia wanaripotiwa kutumikishwa vitani na waasi nchini humo.

Bwana Van der Klaauw amesema hayo akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, huku akiongeza kwamba wengi wa wahamiaji hawana habari ya vita vinavyoendelea nchini humo kabla ya kufikia kwenye boti zinazowavukisha kwenda Yemen. Hata hivyo amesema wengi wao wanajaribu kuvuka Yemen na kufika Saudia, lakini safari hiyo ni hatari mno.

Kwa mujibu wa UNHCR, wahamiaji 92,000 wamewasili Yemen mwaka 2015 licha ya mzozo.

Bwana Van der Klaauw akataja harakati zinazotakiwa kuchukuliwa ili kupunguza wimbi la wahamiaji na hatari wanazokumbana nazo.

(Sauti ya Bwana Van der Klaauw)

“ Kuanzisha fursa bora za kuishi na kukuza utulivu nchini mwao, kuelimisha watu kabla hawajasafiri kuhusu wanachoweza kutarajia Yemen au kwingineko ili wafikirie upya. Pia tumewekeza katika kuimarisha uwezo wa vikosi vya usalama baharini ili kuokoa watu.”