Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apokea tuzo kutoka Hispania, aiomba isaidie utatuzi wa mizozo

Ban apokea tuzo kutoka Hispania, aiomba isaidie utatuzi wa mizozo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepokea tuzo kuhusu masuala ya kiuchumi huko Hispania na kushukuru nchi hiyo kwa kutambua dhima ya Umoja wa Mataifa katika kujenga maendeleo, kulinda amani na utetezi wa haki za binadamu. Bwana Ban amesema Hispania imekuwa mshirika wa karibu wa Umoja wa Mataifa katika ajenda mbali mbali kuanzia maendeleo, usaidizi wa kibinadamu hadi ulinzi wa amani na ameomba ushirikiano hao uendelee kwa maslahi ya dunia nzima. 

(SAUTI YA BAN)

Tunahitaji ukarimu wenu kushughulikia hali mbaya inayozidi kuzorota Syria, na mzozo huko Mali na  ukanda wa Sahel. Tunahitaji mtuunge mkono ili kuendeleza utulivu eneo la Mediteranian na Mashariki ya Kati. Tunahitaji ufadhili wenu katika mpango wa Umoja wa mataifa ya utamaduni wa kiustaarabu, jitihada zetu za kukabiliana na misimamo mikali na kuendeleza maelewano baina ya watu na mataifa yote vile vile.”