Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji muhimu yafikia walionaswa kwenye mapigano Madaya, Syria

Mahitaji muhimu yafikia walionaswa kwenye mapigano Madaya, Syria

Nchini Syria, hatimaye msafara wa magari yaliyobeba bidhaa muhimu za kuokoa maisha ya watu wanaokumbwa na njaa umewasili kwenye mji wa Madaya nchini humo. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Shehena ni pamoja na vifaa vya tiba, vyakula na mablanketi kutoka Umoja wa Mataifa na washirika wake na lengo ni kufikia wakazi 42,000 ambao wameripotiwa kukumbwa na njaa kutokana na eneo lao kuzingirwa na vikosi vinavyounga mkono serikali.

Akihojiwa na redio ya Umoja wa MAtaifa hii leo, Mratibu wa maswala ya kibinadamu nchini Yemen Yacoub El-Hillo amezungumzia kile alichoshuhudia alipofika Madaya na msafara wa msaada.

(Sauti ya Bwana El-Hillo)

"Tuliona maelfu ya watu walioko katika hali ngumu, maelfu walio wanyonge, na watoto walio na utapaimlo uliokithiri, tuliona wazee ambao walikuwa katika hali tete ya kiafya kwa sababu ya ukosefu wa upatikanaji wa chakula. Na tuliona watu ambao wanaonekana kupoteza matumaini."

Kwa mujibu wa OCHA watu 400,000 wanakumbwa na utampiamlo wa kupindukia kwenye maeneo yaliyozingirwa, wengine wakiwa hatarini kufa kwa njaa.