Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya watoto Yemen si shwari:UNICEF

Hali ya watoto Yemen si shwari:UNICEF

Wakati hamna dalili yoyote ya kukomesha vita nchini Yemen, takriban watoto milioni 10 ndani ya nchi hiyo wametangulia mwaka mpya katika machungu na mateso, limesema Shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia watoto, UNICEF. John Kibego na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Kibego) 

Mwakilishi wa UNICEF huko Yemen Julien Harneis, amesema, mashambulio ya mabomu yasiokoma na mapigano kwenye mitaa vimewaweka wazi kwa vurugu, magonjwa na kunyimwa haki zingine.

Ameongeza kuwa athari ya moja kwa moja ni ngumu kubaini, lakini takwimu za umoja wa mataifa zinazosema kuwa watoto 747 waliuauwa na wengine 1,108 walijeruhiwa tangu Machi mwaka jana, na 724 walitumikishwa katika aina tofauti ya harakati za kijeshi ni ishara ya uzito wa mzozo huo kwa watoto.

UNICEF imesema watoto wanachangia nusu ya watu milioni 2.3 wanaokadiriwa kukimbia makwao, na zaidi ya milioni 19 wanaokabiliwa na changamoto ya kupata maji huku watoto milioni 1.3 wakikabiliwa vibaya na utapiamlo.