Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya wahamiaji kuongezeka kwa kasi, wana mchango mkubwa kiuchumi: DESA

Licha ya wahamiaji kuongezeka kwa kasi, wana mchango mkubwa kiuchumi: DESA

Ripoti ya mwaka kuhusu wahamiaji iliyotolewa leo na idara ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA, inaonyesha kuwa kasi ya ongezeko la wahamiaji kimataifa ni kubwa kuliko kasi ya ongezeko la idadi ya watu duniani. Flora Nducha na maelezo  kamili.

(Taarifa ya Flora)

Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa Mkuu wa kitengo cha wahamiaji na  idadi ya watu katika DESA Bela Hovy amesema kuwa idadi ya wahamiaji inaonyesha ongezeko la mahitaji na uwezo wao wa kuhamahama na kwamba dunia inapaswa kujiandaa.

Hata hivyo Bwana Hovy amesema wahamaiji wana mchango mkubwa katika uchumi hususani katika nchi zinazoendelea

(SAUTI HOVY)

‘‘Kuna michango mingi inayotolewa na wahamiaji katika nchi walizofikia na watokako mathalani mwak 2014 benki ya dunia ilikadiria kuwa wahamiaji walituma zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 400 kwa familia zao katika nchi zinazoendelea. Hii ni mara tatu ya miasaada ya maendeleo.’

Amesema kumekuwa na mtizamo hasi kuwa wakimbizi wanaosaka hifadhi kutokana na machafuko mathalani Mashariki ya Kati na Afrika wanafanyakosa jambno alilosema nikitendo halali lakini akatahadhrisha kuwa idadi yao miongoni mwa wahamiaji inakuwa na hivyo dunia yapaswa kuwa makini.