Katibu Mkuu atoa ujumbe wa uchaguzi CAR

29 Disemba 2015

Kuelekea uchaguzi wa rais na wa bunge tarehe 30 Disemba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA unaendelea na maandalizi, leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa ametoa ujumbe kwa raia wa CAR.

Kwenye ujumbe huo uliosambazwa na redio ya Umoja wa Mataifa nchini humo Guira FM, Katibu Mkuu ameelezea mshikamano wake na raia wa CAR.

(Sauti ya Bwana Ban)

“ Uchaguzi unaokuja ni wakati wa kihistoria kwa nchi yenu. Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati hawajawahi kujiandikisha kupiga kwa kiasi hicho. Nawaomba wote mutmie haki yenu ya kupiga kura. Msiache wengine kuwazuia kujielezea huru.”

Aidha MINUSCA imeitisha leo mkutano wa wagombea urais pamoja na Tume ya Uchaguzi kujadili mchakato wa uchaguzi na usalama wake, usambazaji wa vifaa vya uchaguzi na makaratasi ya kupiga kura ukiendelea nchini humo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter