Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guinea sasa haina tena maambukizi ya Ebola:WHO

Guinea sasa haina tena maambukizi ya Ebola:WHO

Shirika la afya duniani leo limetangaza kumalizika kwa maambukizi ya virusi vya Ebola katika Jamhuri ya Guinea. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA HASSAN)

Ni siku 42 zimepita tangu mtu wa mwisho kuthyibitika kuwa na homa ya virusi vya Ebola kupimwa na kutokutwa na virusi hivyo kwa mara ya pili.

Guinea sasa inaingia katika siku 90 za uangalizi kuhakikisha kwamba visa vyovyote vipya vinabainiwa haraka kabla havijasambaaa kwa watu wengine. Tarik Jašarević ni afisa habari wa WHO.

(SAUTI YA TARIK JUSAREVIC)

WHO imeipongeza serikali na watu wa Guinea kwa mafanikio hayo makubwa ya kukomesha mlipuko wa Ebola.

Kwa mujibu wa WHO hii ni hatua muhimu saana kwa kwa mlipuko wa Ebola Afrika ya Magharibi ikizingatiwa kuwa mzunguko wa maambukizi ya virusi hivyo ulianzia Gueckedou Guinea miaka miwili iliyopita mwisho wa Desemba 2013, na kusambaa katika nchi jirani za Liberia na Sierra Leone na hatimaye kupitia nchi kavu na njia ya anga kusafiri hadi mataifa mengine saba duniani.