Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

GAVI na wadau waja na mbinu mpya kudhibiti magonjwa kupitia chanjo

GAVI na wadau waja na mbinu mpya kudhibiti magonjwa kupitia chanjo

Ubia wa chanjo duniani  GAVI, umekuja na mkakati dhidi ya magonjwa yanayoweza kupatiwa kinga kwa njia ya chanjo ambapo nchi masikini zinatarajiwa kunufaika.

Akiongea mjini Geneva mwakilihsi wa GAVI Dk Seth Berkley amesema surua ndiyo kipaumbele katika mbinu hiyo mpya ambapo GAVI itashirikiana na serikali katika nchi 73 masikini duniani nyingi zikiwa ni kutoka barani Afrika.

Amesema kiasi cha dola milioni 800 kitatumika ikiwa ni uwekezaji unaotarajiwa kuokoa vifo vya watoto milioni moja. Kuhusu namna watakavyoendesha zoezi hilo anasema.

(SAUTI DK SETH)

‘Tunafanaya kazi kupitia serikali, kwasababu chanjo ni huduma ya kijamii inayotolewa na serikali. Sio kila sehemu tunafanya kazi na serikali mfano Somalia na sehemu ambazo kuna kiwango kikibwa cha rushwa na hakuna mifumo thabiti. Katika maeneo hayo tunafanya kazi na washirika wetu mathalani WHO na UNICEF.’’

Hata hivyo Dk Seth amesema kwamba  nchi zilizoendelea pia zinakabiliwa na surua na zitajumuishwa katika mkakati huo ikiwamo Marekani, Canada, Uswisi, Australia na , Uingereza.