Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yaelezea matarajio yake kwenye COP20

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa 20 wa mabadiliko ya tabianchi huko Lima, Peru. (Picha@Everline Mkokoi-VPO)

Tanzania yaelezea matarajio yake kwenye COP20

Tanzania imesema hakikisho la usaidizi wa fedha, teknolojia na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni moja ya mambo makuu matatu ambayo inatarajia kuwa yatajadiliwa kwa kina huko Peru kwenye kikao cha COP20 na hatimaye kujumuishwa kwenye mkataba wa mabadiliko ya tabianchi baadaye mwakani huko Paris.

Akizungumza na Idhaa ya Radio ya Umoja wa Mataifa kutoka Lima, Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kwenye ofisi ya Makamu wa Rais nchini Tanzania, Richard Muyungi ametaja jambo lingine utekelezaji wa ahadi ya dola Bilioni 9.6 kwenye mfuko wa mabadiliko ya tabianchi.

(Sauti ya Muyungi)

Jambo la tatu ni kuhakikisha utoaji wa hewa chafuzi unadhibitiwa ambapo alipoulizwa kuwa ahadi za hivi karibuni kutoka China na Marekani siyo za kisiasa, Bwana Muyungi amesema.

(Sauti ya Muyungi)