Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wa raia wa Sudan Kusini wasaka hifadhi DRC.

Maelfu wa raia wa Sudan Kusini wasaka hifadhi DRC.

Zaidi ya watu 4000 nchini Sudan Kusini wamefurushwa makwao na kusaka hifadhi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , DRC kufuatia mapigano ya hivi karibuni kati ya kikundi kifahamikacho kwa jina la vijana wa mkuki dhidi ya jeshi la nchi hiyo. John Kibego na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Kibego)

Kwa mujibu wa UNHCR, hadi sasa timu ya shirika hilo imeshaandikisha wakimbizi zaidi ya 3,000 ambao wamewasili mpakani, idadi hiyo ikiwa ni ya juma hili pekee.

Timu hiyo imeripoti kuwa zaidi ya wakimbizi Elfu Moja wa  DRC waliokuwa Sudan Kusini sasa wamekimbilia eneo hilo la Mashariki mwa DRC kukwepa machafuko, huku pia zoezi la usajili likiendelea mpakani mwa nchi hizo.

Machafuko nchini Sudan Kusini yaliyolipuka miaka miwili iliyopita mjini Juba yamesababisha hadi sasa watu zaidi ya milioni mbili kukimbia makazi yao.

Margareth Loej [LOY] ni mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na anaeleza kile kinachopaswa kufanya kurejesha amani nchini humo.

(Sauti ya Margaret)

“Matumaini nchini Sudan Kusini ni kutekelezwa kwa mkataba wa amani uliotiwa saini na pande kinzani mwezi Agosti, na jamii ya kimataifa na ukanda na nchi jirani zinapaswa kusaidia utekelezaji huo.”