Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za vyakula zashuka mwezi Novemba

Bei za vyakula zashuka mwezi Novemba

Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO limesema bei za vyakula zimeshuka mwezi wa Novemba, zikiwa zimepungua kwa asilimia 18 ikilinganishwa na bei za Novemba mwaka jana.

Hata hivyo, FAO imeonya kwamba licha ya kushuka kwa bei, hali ya uhakika wa chakula imezidi kuwa mbaya kwenye maeneo yaliyokumbwa na mizozo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo.

Kwenye nchi 33, nyingi zikiwa barani Afrika, watu wamekumbwa na upungufu wa chakula kwa sababu ya ukame au mafuriko yaliyosababishwa na El-Niño, au mizozo.

Aidha ripoti imeonyesha kwamba licha ya bei ya sukari kuendelea kupanda kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bei za vyakula vyote zimepungua, kutokana na thamani kubwa ya dola na uwepo wa vyakula kwa wingi.