Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna muda wa kupoteza, lazima dunia iafikiane kuhusu tabianchi: Ban

Hakuna muda wa kupoteza, lazima dunia iafikiane kuhusu tabianchi: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mchakato wa makubaliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi  katika mkutano unaoendelea  mjini Paris Ufaransa unatia moyo na kwamba hakuna muda wa kupoteza wala mbadala wa kuafikiana.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bwana Ban amesema kwa muda mrefu dunia imekuwa haina makubaliano jumuishi kuhusu hali ya hewa lakini akaonya bado kuna mengi ya kufanya .

(SAUTI BAN)

‘Katika uchumi wa dunia, mpito wa mustakabali wa kupunguza hewa chafuzi unaendelea. Katika chumba cha majadiliano kuna kazi kubwa ya kufanya. Mambo muhimu bado hayajapitiwa suluhu, na hakuna muda uliosalia. Naendelea kutoa msukumo kwa nchi zilizoendelea kutambua wajibu wao katika kuongoza, na kuzitaka nchi zinazoendelea kufanya zaidi kuhusu uwezo wao unaokuwa.’’

Katibu Mkuu pia amezungumzia janga la wakimbizi, wahamaiaji na ugaidi akisema ni ajenda inayogonga vichwa duniani kwa sasa, na kuongeza kuwa juhudi za kimataifa ziimarishwe kwa kuzingatia haki za binadmau kwani hofu haipaswi kutawala dunia.

Ban akasisitiza zaidi kuhusu ugaidi akisema asilimia kubwa ya vitendo hivyo ni matokeo ya mgogoro wa Syria ambapo ana matuamaini  kuwa juhudi za upatanishi dhidi ya pande kinzani zitazaa matunda akiangazia majadiliano ya amani ya Vienna. Amesema mgogoro wa Syria umezaa madhila kadhaa.

(SAUTI BAN)

‘Katika kipindi cha miaka mitanao tangu kaunza kwa mgogoro huu wa Syria  majanga makubwa yametokea, ikiwamo mamilioni ya wakimbizi, watu takribani milioni 13 ndani ya Syria wanahitaji msaasa wa kibinadamu wa dharura. Tumeteseka na kujitoa kwa ajili ya kusambaa kwa ugaidi na vikundi vyenye misimamo mikali.’’

Katika hatau nyingine Katibu Mkuu amemteua Bwana Ghassim Wane wa Mauritania kuwa msaidizi wake katika operesheni za ulinzi wa amani pamoja na Dk David Nabarro kuwa mshauri maalum wa ajenda ya 2030 ya maendeleo  endelevu.