Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya vijana ndani ya COP21 ni muhimu: Alhendawi

Siku ya vijana ndani ya COP21 ni muhimu: Alhendawi

Mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 umeingia siku ya nne hii leo huko Paris, Ufaransa ambapo kumemefanyika tukio la siku ya vijana na kizazi kijacho likiangazia vijana na nafasi yao katika kukabili mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, Ahmed Alhendawi amesema vijana kote ulimwenguni wana matarajio makubwa juu ya makubaliano yatakayofikiwa na kwamba tukio la leo..

(Sauti ya Alhandawi)

 “Kwangu mimi haya ni matukio ya kwa nini tunapaswa kuchagiza mchakato wa mashauriano na kufikia makubaliano. Siku ya vijana inatukumbusha na kuonyesha udharura wa mashauriano na nitaendelea kusihi watu  kupaza sauti zao na kutumia siku hii kama jukwaa la kukumbusha kila mtu kuwa kile kinachopaswa kuamuliwa sasa ni kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.”

Amesisitiza kuwa vijana wanafuatilia kwa makini mashauriano yanayoendelea na wametumia siku hiyo kupaza sauti zao.