Tumepiga hatua mapambano dhidi ya kipindupindu: Tanzania

30 Novemba 2015

Harakati za kupambana na ugonjwa kipindupindu nchini Taanzania uliosababisha vifo vya wagonjwa takribani 150 zimeanza kuzaa matunda kutokana na kupungua kwa idadi ya visa vipya.

Takwimu za shirika la agya ulimwenguni WHO na serikai ya Tanzania zineonyesha kuwa zaidi ya wagonjwa elfu tisa wameambukizwa.

Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini humo Dkt. Janeth Mghamba ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa malengo ya kudhiti kipindupindu ifikapo mwishoni wa mwezi Desemba yatatatimia.

(SAUTI DK JANETH)

Amesema hata hivyo idadi ya vifo imevuka asilimia moja ambayo ni dalili za kukithiri kwa ugonjwa,hii ikiwa ni kwa mujibu wa viwango vya WHO

Idadi ya mikoa yenye maambukizi ya kipindupindu nchini Tanzania ni 19 hadi sasa .

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter