Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kina cha bahari chaathiri wakulima Vietnam

Kina cha bahari chaathiri wakulima Vietnam

Kuongezeka kwa kina cha bahari ambayo ni sehemu ya mabadiliko ya tabianchi kunaathiri wakulima wa mazao mbalimbali duniani mathalani nchini Vietnam.

Ongezeko hilo la kina cha maji linaelezwa kusababishwa na mambo mbali mbali ikiwemo hewa chafuzi ambazo zinasababisha ongezeko la joto duniani na barafu katika ncha ya kaskazini mwa dunia kuyeyuka.

Lakini je huko Vietnam hali ikoje wakati huu ambapo macho na masikio yanaelekezwa huko Paris kwenye mkutano wa COP21. Ungana na Joseph Msami katika makala inayoelezea athari na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kueleta ahueni kwa wakulima.