Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya UNESCO kwa walimu kwa lengo la kuimarisha teknohama

Mafunzo ya UNESCO kwa walimu kwa lengo la kuimarisha teknohama

Shirika la Elimu Sayansi na Utamduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limeendesha warsha ya kutoa mafunzo kwa walimu juu ya teknohama kwa ajili ya kuchukua fursa ambazo zinaendeana na nyakati za dijitali katika karne hii ya ishirini na moja.

Mafunzo hayo ni kufuatia wito uliotolewa nchini China katika kongamano la kimataifa juu ya teknohama na elimu baada ya mwaka 2015, ambako mawaziri wa elimu kutoka nchi mbali mbali walikubaliana kwamba taasisi za kutoa mafunzo kwa walimu zina vifaa vya teknohama ili kupanua nafasi za programu kwa walimu wote.

Shaylor Mwanje ni msaidizi katika kitengo cha habari na mawasiliano UNESCO, Kenya .

(sauti ya Shaylor)

Nchi ambazo zimeshiriki katika mafunzo hayo ni Kenya,Mauritius,Uganda, Ushelisheli na Tanzania.