Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

#WRC15 yafikia ukingoni, nchi za Afrika zanufaika:

#WRC15 yafikia ukingoni, nchi za Afrika zanufaika:

Mkutano wa masafa ya Radio umemalizika huko Geneva, Uswisi ambapo Tanzania na nchi nyingine za ukanda wa Afrika zimepata mafanikio kufuatia masuala muhimu waliyotaka yazingatiwe kuridhiwa.

Akizungumza na idhaa hii, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA Dkt. Ali Yahya Simba akiongoza ujumbe wa nchi yake, ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kulinda masafa ya utangazaji wa dijitali ambayo nchi zilizoendelea zilikuwa zinataka zitumiwe kwa simu za mkononi.

Dkt. Simba akaeleza manufaa kwa mwananchi wa kawaida.

(Sauti ya Dkt. Simba)