Skip to main content

CAR tumieni ziara ya Papa Francis kujenga amani:UNHCR

CAR tumieni ziara ya Papa Francis kujenga amani:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesihi pande kinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kutumia ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani nchini humo, Papa Francis kama fursa ya kujenga amani na maridhiano na hatimaye kuruhusu mchakato wa kisiasa kukamilika.

Papa Francis anatarajiwa nchini humo Jumapili ambapo UNHCR imesema hatua hiyo itakuwa ni muhimu kutokana na mapigano baina ya jamii tofauti zilizosababisha ongezeko kwa asilimia 18 la watu waliopoteza makazi.

Ghasia hizo pia zimesababisha kuahirishwa kwa chaguzi za Rais na wabunge zilizokuwa zifanyike Oktoba 18 na sasa matarajio ni kuwa zitafanyika Disemba 27.

Leo Dobbs ni msemaji wa UNHCR Geneva, Uswisi.

“Ijapokuwa hali kwenye mji mkuu Bangui ni tulivu lakini tete, tuna wasiwasi  na mlipuko wa ghasia nchini CAR ambao umekwamisha juhudi za kurejesha amani ya kudumu na halikadhalika kuweka hatarini chaguzi za mwezi Disemba.