Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu la kisiasa ndiyo muarubaini wa usalama: Ban

Suluhu la kisiasa ndiyo muarubaini wa usalama: Ban

Baraza la usalama leo limekutana kujadili udumishaji wa amani na usalama kwa kuangalia mustakhabali wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaeleza washiriki kuwa  gharama za machafuko kisiasa, na kibinadamu zinaongezeka huku ukosefu wa suluhu ukizaa ukosefu wa usalama, ukosefu wa haki na mateso kwa mamilioni ya watu leo.

Ban amesema mahitaji ya kutatua  migogoro yanasababaisha mzigo mkubwa katika vyombo vya amani na usalama hususani operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifam, lakini akasisitiza.

(SAUTI BAN)

‘Opersheni za amani ni vyombo vya  kisiasa. Zinawekwa nanyi ili kusaidia utulivu wa kisiasa katika mgogoro. Ni ishara ya jukumu la  jumuiya ya kimataifa katika kusaidia kusaka na kudumisha suluhu la kisiasa.’’

Wachangiaji wengine katika mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wamesisitiza kuwa suluhu la kisiasa ni muhimu katika kutatua mizozo hususani sehemu ambazo vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa vimepelekwa.