Skip to main content

Masafa ya radio yatengwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa ndege

Masafa ya radio yatengwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa ndege

Makubaliano yamefikiwa na mkutano mkuu wa masafa ya radio kwa ajili ya kutenga masafa maalumu ya kufuatilia ndege popote pale ikiwemo katika maeneo ya juu ya maji. Mkutano huo umetenga masafa maalum kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kutoka kwenye  ndege hadi kwenye setelaiti, hii ni kwa ajili ya ufuatiliaji wa ndege.

Katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Idhaa hii Innocent Mungy ambaye ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano  nchini Tanzania ameelezea maana ya makubaliano hayo. Kwanza anaeleza sababu ya kutenga masafa kufanyika mapema.

(mahojiano)