Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dr Anna Tibaijuka afafanua ripoti ya ukuaji wa miji, makazi na mitaa ya mabanda

Dr Anna Tibaijuka afafanua ripoti ya ukuaji wa miji, makazi na mitaa ya mabanda

Mkutano wa tano kuhusu hali ya miji na makazi umeanza mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, ukijumuisha washiriki kutoka kila pembe ya dunia.

Mkutano huo unafuatia ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-Habitat ya ukuaji wa miji na mitaa ya mabanda. Na umeandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Brazilin na UN-Habitat. Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kutafuta suluhu la ongezeko la matatizo uya ukuaji wa miji.

Kauli mbiu mwaka huu ni "Haki ya kuishi mjini na kuondoa mgawanyiko". Pia unaelimisha jamii ni kwa nini malioni ya watu kila mwaka hukimbilia mijini kutoka vijijini.

Ripoti ya UN-Habitat inasema idadi ya watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabada imepungua japo katika maeneo mengine inaonekana kuongezeka. Mkurugenzi mkuu wa UN-Habitati Dr Anna Tibaijuka anafafanua kuhusu ripoti hiyo.