Tutazijengea uwezo taasisi za sayansi :UNESCO
Kamisheni ya sayansi asilia ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, imekuwa na mjadala kuhusu sayansi kimataifa ili kuleta maendeleo endelevu ambapo pamoja na mambo mengine imeazimia kuzijengea uwezo taasisi za masuala ya sayansi duniani.
Mwakilishi wa Tanzania ambaye ni Katibu Mkuu wa tume ya taifa ya UNESCO nchini humo Dk Moshi Kimizi nayehudhuria mkutano mkuu wa shirikia hilo mjini Paris Ufaransa ameiambia idhaa hii kuwa mambo mengine yaliyokubaliwa na tume hiyo ili kukuza sanyansi ni.
(SAUTI KIMIZI)
Kadhalika kamisheni imesisisiza kuwa kwa kuwa sayansi ni suala mtambuka , tasina hiyo itumiwe na kila jamii katika kuhakikisha maendeleo.