Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa intaneti katika kutekeleza SDGs kumulikwa Brazil

Umuhimu wa intaneti katika kutekeleza SDGs kumulikwa Brazil

Watu takribani 5,000 wakiwamo maafisa wa ngazi za juu wa serikali, viongozi wa asasi za kiraia na wataalamu wa sera za intaneti wanakutana nchini Brazil kuanzia Novemba 10 hadi 13 katika mkutano wa 10 wa jukwaa la utawala wa intaneti (IGF) , kujadili jukumu muhimu la mtandao huo  katika kufanikisha utekelezaji wa ajenda 2030 ya malengo endelevu.

IGF inakuja wakati ambapo malengo ya maendeleo endelvu yamepitishwa hivi karibuni ambayo yanasisitiza umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano na intaneti katika shughuli za maendeleo.

Ajenda 2030 pia ni muhimu katika kuongeza upatikanaji teknolojia ya habari na mawasiliano na katika upatikanaji wa kimataifa wa intanenti kwa nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2020.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hivi karibuni amenukuliwa akiangazia umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika utekelezaji wa ajenda 2030.