Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa gesi chafuzi waweka rekodi mpya

Uzalishaji wa gesi chafuzi waweka rekodi mpya

Kiwango cha gesi chafuzi angani kilifikia rekodi mpya mwaka 2014, kikiashiria kuendeleza ongezeko la uzalishaji wa gesi hizo zinazochangia mabadiliko ya tabianchi, limesema Shirika la Hali ya Hewa Duniani, WMO.

Katika ripoti yake mpya kuhusu gesi, WMO imesema kuwa kuongezeka viwango vya gesi chafuzi kutafanya sayari dunia kuwa hatarishi zaidi na isiyoweza kukaliwa na vizazi vya siku za usoni.

WMO imesema katika muongo mmoja uliopita, gesi ya mkaa au kaboni imechangia kwa asilimia 83 ongezeko la uchafuzi angani.

Michel Jarraud in katibu Mkuu wa WMO

Hatuna fursa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi tusipokabiliana na uzalishaji wa gesi ya mkaa. Ni muhimu kuchukua hatua haraka, kwa sababu tusipochukua hatua haraka, tunachozalisha kitaathiri kizazi kijacho. Takriban robo ya gesi chafuzi zinavutwa na bahari, robo nyingine na ardhi na takriban asilimia 50 zinasalia angani. Na zinasalia kwa muda mrefu sana.”