Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanataaluma wote duniani watambuliwe:UNESCO

Wanataaluma wote duniani watambuliwe:UNESCO

Kutambulika kwa wanataaluma duniani bila kujali eneo wanalotoka ni moja ya ajenda zilizochukua nafasi katika mjadala kuhusu kamisheni ya elimu kupitia Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO unaoendelea mjini Paris, Ufaransa.

Mjadala huo wa mwishoni mwa juma unafuatia mkataba wa elimu uliotiwa saini nchini Ethiopia takbribani miezi saba iiyopita. Katika mahojiano na idhaa hii Katibu Mtendaji wa UNESCO nchini Tanzania Dk. Moshi Kiminzi anayehudhuria mkutano huo anaelezea faida ya mkataba huo.

(SAUTI KIMINZI)

Kadhalika mkutano huo umejadili miundo mkakati ya UNESCO katika kubadili dunia katika mtazamo mzima wa elimu.