Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Theluthi moja ya watu duniani hukumbwa na vizuizi vya moja kwa moja

Theluthi moja ya watu duniani hukumbwa na vizuizi vya moja kwa moja

Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na vizuizi Idriss Jazairy ametoa wito leo kwa nchi wanachama ziache kutumia vizuizi vya moja kwa moja akisema theluthi moja ya watu duniani kote wanaishi kwenye nchi zinazokumbwa na vizuizi hivyo.

Akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bwana Jazairy amesisitiza gharama za vizuizi hivyo kwa haki za watu wanaoishi kwenye mazingira magumu zaidi.

Ameziomba nchi hizo kuachana na vizuizi vya moja kwa moja na kufuatilia miongozo ya Baraza la Usalama ya kupendekeza mazungumzo ya pamoja kuhusu vizuizi na kutoweka vizuizi dhidi ya vifaa vya usaidizi wa kibinadamu.