Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushahidi unaopatikana kwa njia ya mateso upuuzwe:UM

Ushahidi unaopatikana kwa njia ya mateso upuuzwe:UM

Mtaamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya mateso ametaka ushahidi unaopatikana baada ya kufanyika vitendo vya kuwatesa watuhumiwa usipewe uzito wowote tena.

Akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mtaalamu huyo Juan Mendez amesema hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa ili kukomeshwa kwa hali hiyo ya kuwatesa watuhumiwa.

Ameeleza kuwa taarifa zozote za kiushahidi ambazo zinachukuliwa na waendesha mashtaka baada ya kuendesha vitendo vya mateso lazima zianze kuzembewa kwani hatua hiyo haifungamani na haki za msingi za binadamu na pia kuyaendekea kinyume matakwa ya msingi ya binadamu.