Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha ahadi ya Netanyahu kudumisha hali ya eneo takatifu Jerusalem

Ban akaribisha ahadi ya Netanyahu kudumisha hali ya eneo takatifu Jerusalem

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha taarifa ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiahidi kuwa atadumisha hali ilivyokuwa zamani kwenye eneo takatifu la Haram al Sharif au Temple Mount kule Jerusalem, kwa maneno na kwa vitendo.

Amezingatia ahadi ya Waziri huyo Mkuu kuwa Israel haina nia yoyote ya kugawanya eneo hilo takatifu, na kwamba inaheshimu umuhimu wa mchango wa Ufalme wa Jordan, kama ilivyobainika katika mkataba wa amani wa 1994 kati ya Jordan na Israel, na mchango wa kihistoria wa Mfalme Abdullah II.

Katibu Mkuu anatarajia kuwa kuimarishwa kwa utaratibu wa kiusalama kati ya Israel na Wakf wa Jordan utachangia kuhakikisha kuwa wageni na waabudu wanaonyesha utulivu na kuheshimu utakatifu wa eneo hilo.