Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa kibinadamu Yemen ataka pande kinzani ziwalinde raia

Mratibu wa kibinadamu Yemen ataka pande kinzani ziwalinde raia

Mratibu wa kibinadamu nchini Yemen, Johannes Van Der Klaauw, ametoa wito kwa pande kinzani nchini humo ziyalinde maisha na haki za raia.

Bwana Van Der Klaauv amesema kuwa vita nchini humo vinasababisha gharama kubwa kwa raia, ama kupitia kwa vitendo vya pande kinzani, au vizuizi vya uagizaji bidhaa za biashara, ambavyo vimefanya taasisi zinazotoa huduma muhimu kushindwa kupata vifaa kazi muhimu.

Tangu kuchacha kwa mgogoro mnamo mwezi Machi, zaidi ya watu 2,500 wamuawa na zaidi ya watu 5,000 kujeruhiwa nchini Yemen.

Mratibu huyo wa kibinadamu amesema huduma muhimu zilizodhoofika, zikiwemo za afya, maji na kujisafi, zipo karibu kusambaratika kabisa, huku mamilioni ya raia wa Yemen wakihitaji kwa msaada wa chakula, na usaidizi wa lishe kwa watoto wao.