Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za barabarani zazidi kuchukua uhai katika nchi maskini

Ajali za barabarani zazidi kuchukua uhai katika nchi maskini

Takribani watu Milioni Moja nukta Tatu hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, wengi wao wakiwa wakazi wa nchi maskini, imesema ripoti mpya ya hali ya usalama barabarani iliyotolewa leo na shirika la afya duniani, WHO ikisema ongezeko linazidi kila mwaka licha ya kuimarishwa kwa usalama barabarani.

Ripoti inasema vifo vimeongezeka katika nchi 68 ilihali vimepungua katika nchi 79 ambapo WHO inasema hatari ya kufariki dunia kwenye ajali barabarani duniani inategemea eneo ambalo mtu huyo, kiwango kikiwa kikubwa zaidi Afrika ikilinganishwa na Ulaya.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amepongeza nchi zilizopunguza vifo kutokana na ajali barabarani akisema..

(Sauti ya Dkt. Chan)

"Kwa kutumia taarifa kutoka nchi 180, ripoti inaonyesha kiwango cha vifo kwa mwaka kutokana na ajali za barabarani kimesalia palepale na nchi ambazo zimefanikiwa zaidi katika kupunguza vifo vinavvyotokana na ajali za barabarani, zimefanikiwa kutokana na uboreshaji wa sheria na usimamizi na kuhakikisha barabara na magari ni salama.”

WHO inasema nchi zimechukua hatua kudhibiti usalama barabani ikiwemo kuzingatia matumizi ya mikanda, udhibiti wa mwendo kasi na unywaji pombe lakini usimamizi wa kanuni hizo unatakiwa zaidi.